Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mnanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa?
Yobu 8:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jifunze tafadhali kwa wale waliotutangulia, zingatia mambo waliyogundua hao wazee. Biblia Habari Njema - BHND Jifunze tafadhali kwa wale waliotutangulia, zingatia mambo waliyogundua hao wazee. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jifunze tafadhali kwa wale waliotutangulia, zingatia mambo waliyogundua hao wazee. Neno: Bibilia Takatifu “Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini, Neno: Maandiko Matakatifu “Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini, BIBLIA KISWAHILI Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; |
Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mnanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa?
Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto uaminifu wako.
Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi. Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu?
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.
Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiwa na miisho ya nyakati.
Kumbuka siku za kale, Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonesha; Wazee wako, nao watakuambia.
Tazama siku zilizopita, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile Mungu aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na kutoka pembe hii ya mbingu hadi ile, kama kumetukia neno lolote kama neno hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili?