La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Yobu 8:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Tazama! Mungu hatamkataa mtu asiye na hatia, wala kuwasaidia waovu. Biblia Habari Njema - BHND “Tazama! Mungu hatamkataa mtu asiye na hatia, wala kuwasaidia waovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Tazama! Mungu hatamkataa mtu asiye na hatia, wala kuwasaidia waovu. Neno: Bibilia Takatifu “Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia, wala kuitia nguvu mikono ya mtenda maovu. Neno: Maandiko Matakatifu “Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia, wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya. BIBLIA KISWAHILI Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. |
La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali?
Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.