Lakini sasa amekufa nifungie nini? Je! Naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi.
Yobu 7:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ndivyo alivyo huyo ashukaye kuzimuni, hatazuka tena kabisa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama wingu lififiavyo na kutoweka ndivyo nao watu washukavyo kuzimu bila kurudi. Biblia Habari Njema - BHND Kama wingu lififiavyo na kutoweka ndivyo nao watu washukavyo kuzimu bila kurudi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama wingu lififiavyo na kutoweka ndivyo nao watu washukavyo kuzimu bila kurudi. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini harudi tena. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini harudi tena. BIBLIA KISWAHILI Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ndivyo alivyo huyo ashukaye kuzimuni, hatazuka tena kabisa. |
Lakini sasa amekufa nifungie nini? Je! Naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi.
Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyoweza kuzoleka tena; wala Mungu haondoi maisha ila hufikiri shauri, kwamba yeye aliyefukuzwa asiwe mkimbizi kwake.
Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?
Vitisho vimenigeukia; Huifukuza heshima yangu kama upepo; Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.
Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.
Nilisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.