Yakobo baba yao akawaambia, Mmeniondolea watoto wangu; Yusufu hayuko, wala Simeoni hayuko, na Benyamini mnataka kumchukua naye; mambo hayo yote yamenipata mimi.
Yobu 7:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kumbuka, maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona jema lolote tena. Biblia Habari Njema - BHND “Kumbuka, maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona jema lolote tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kumbuka, maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona jema lolote tena. Neno: Bibilia Takatifu Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi; macho yangu kamwe hayataona tena raha. Neno: Maandiko Matakatifu Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi; macho yangu kamwe hayataona tena raha. BIBLIA KISWAHILI Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena. |
Yakobo baba yao akawaambia, Mmeniondolea watoto wangu; Yusufu hayuko, wala Simeoni hayuko, na Benyamini mnataka kumchukua naye; mambo hayo yote yamenipata mimi.
Nakuomba, likumbuke neno lile ulilomwamuru Musa, mtumishi wako, ukisema, Mkikosa, nitawatawanya kati ya mataifa;
Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
Kweli, watu wote hupita kama kivuli; Wao hujisumbua bure tu; Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.
Ukumbuke, Ee Bwana, Wanavyosimangwa watumishi wako; Jinsi ninavyostahimili kifuani mwangu Masimango ya watu wengi.
Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.
lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.