Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata.
Yobu 7:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu kuongea; nitasema kwa msongo wa roho yangu, nitalalamika kwa uchungu wa nafsi yangu. Biblia Habari Njema - BHND “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu kuongea; nitasema kwa msongo wa roho yangu, nitalalamika kwa uchungu wa nafsi yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu kuongea; nitasema kwa msongo wa roho yangu, nitalalamika kwa uchungu wa nafsi yangu. Neno: Bibilia Takatifu “Kwa hiyo sitanyamaza; nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu. Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa hiyo sitanyamaza; nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu. |
Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata.
Nayachukia maisha yangu; Nitayasema malalamiko yangu wazi; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
Mimi nikiwa mwovu, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Maana nimejaa aibu Nikiyaangalia mateso yangu.
Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi; Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?
Moyo wangu ukawa moto ndani yangu, Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka; Nilisema kwa ulimi wangu,
Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa. Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.
Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.
Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Maana katika dhiki nyingi na taabu ya moyo niliwaandikia nikiwa na machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.