Wewe unafanya upya ushahidi wako juu yangu, Na kuongeza kisirani chako juu yangu; Ukileta jeshi baada ya jeshi juu yangu.
Yobu 7:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Mtu hana huduma ngumu juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Binadamu anayo magumu duniani, na siku zake ni kama siku za kibarua! Biblia Habari Njema - BHND “Binadamu anayo magumu duniani, na siku zake ni kama siku za kibarua! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Binadamu anayo magumu duniani, na siku zake ni kama siku za kibarua! Neno: Bibilia Takatifu “Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani? Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa? Neno: Maandiko Matakatifu “Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani? Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa? BIBLIA KISWAHILI Je! Mtu hana huduma ngumu juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? |
Wewe unafanya upya ushahidi wako juu yangu, Na kuongeza kisirani chako juu yangu; Ukileta jeshi baada ya jeshi juu yangu.
BWANA, unijulishe mwisho wangu, Na idadi ya siku zangu ni ngapi; Nijue jinsi maisha yangu yalivyo mafupi.
Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; Wala hakuna kuponyoka katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.
Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, licha ya wingi wa watu wake; na watakaobaki watakuwa wachache sana na dhaifu.
Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari.
Nenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.
Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa jubilii; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo.
Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na BWANA, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.