Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
Yobu 6:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Laiti ningepewa haja yangu, Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Laiti ningejaliwa ombi langu, Mungu akanipatia kile ninachotamani: Biblia Habari Njema - BHND “Laiti ningejaliwa ombi langu, Mungu akanipatia kile ninachotamani: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Laiti ningejaliwa ombi langu, Mungu akanipatia kile ninachotamani: Neno: Bibilia Takatifu “Laiti ningepata haja yangu, kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia, Neno: Maandiko Matakatifu “Laiti ningepata haja yangu, kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia, BIBLIA KISWAHILI Laiti ningepewa haja yangu, Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana! |
Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
Nayachukia maisha yangu; Nitayasema malalamiko yangu wazi; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
Ambao wangojea mauti, lakini hawayapati; Na kuyachimbulia kuliko watafutavyo hazina iliyostirika;
Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!
Basi, sasa, Ee BWANA, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.