Yobu 6:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya; Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nifundisheni, nami nitanyamaza. Nielewesheni jinsi nilivyokosea. Biblia Habari Njema - BHND “Nifundisheni, nami nitanyamaza. Nielewesheni jinsi nilivyokosea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nifundisheni, nami nitanyamaza. Nielewesheni jinsi nilivyokosea. Neno: Bibilia Takatifu “Nifundisheni, nami nitakaa kimya; nionesheni nilikokosea. Neno: Maandiko Matakatifu “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya; nionyesheni nilikokosea. BIBLIA KISWAHILI Nifunzeni, nami nitanyamaza kimya; Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa. |
Tazama, niliyangojea maneno yenu, Nilizisikiliza nisikie hoja zenu, Hapo mlipokitafuta mtakalonena.
Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.