Yobu 6:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji. Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Rafiki zangu wamenidanganya kama kijito, wamenihadaa kama mitaro isiyo na maji. Biblia Habari Njema - BHND Rafiki zangu wamenidanganya kama kijito, wamenihadaa kama mitaro isiyo na maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Rafiki zangu wamenidanganya kama kijito, wamenihadaa kama mitaro isiyo na maji. Neno: Bibilia Takatifu Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa, ni kama vijito vya msimu, ni kama vijito ambavyo hufurika Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa, ni kama vijito vya msimu, ni kama vijito ambavyo hufurika BIBLIA KISWAHILI Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji. Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo. |
Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali.
Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini, Aliyekula pamoja nami, Ameniinulia kisigino chake.
Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.
Kwa maana hata ndugu zako, na nyumba ya baba yako, wamekutenda mambo ya hila; naam, wamepiga kelele nyuma yako; usiwasadiki, wajapokuambia maneno mazuri.
Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha langu halina dawa, linakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?
Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.
Tazama, wanawake wote, walioachwa ndani ya nyumba ya mfalme wa Yuda, watatolewa na kuchukuliwa kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, na wanawake hao watasema, Rafiki zako walio karibu wamekudanganya, nao wamekushinda; na kwa kuwa miguu yako imezama matopeni sasa, wamegeuka na kurudi nyuma.
Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa;