Yobu 5:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema yeye atendaye makuu yasiyochunguzika, atendaye maajabu yasiyohesabika. Biblia Habari Njema - BHND yeye atendaye makuu yasiyochunguzika, atendaye maajabu yasiyohesabika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza yeye atendaye makuu yasiyochunguzika, atendaye maajabu yasiyohesabika. Neno: Bibilia Takatifu Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika. BIBLIA KISWAHILI Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu; |
Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa.
Ni nani huyu afichaye ushauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.
Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Umetuzidishia ila masikio, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!