Yobu 5:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate shida, Kama cheche za moto zirukavyo juu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bali binadamu huzaliwa apate taabu, kama cheche za moto zirukavyo juu. Biblia Habari Njema - BHND Bali binadamu huzaliwa apate taabu, kama cheche za moto zirukavyo juu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bali binadamu huzaliwa apate taabu, kama cheche za moto zirukavyo juu. Neno: Bibilia Takatifu Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, kwa hakika kama cheche za moto zinavyoruka kuelekea juu. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu. BIBLIA KISWAHILI Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate shida, Kama cheche za moto zirukavyo juu. |
Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
Kwa maana mtu hupata nini kwa kazi yake yote, na kwa juhudi ya moyo wake alivyojitahidi chini ya jua?
Kwa kuwa siku zake zote ni masikitiko, na kazi yake ni huzuni; naam, hata usiku moyoni mwake hamna raha. Hayo nayo ni ubatili.
Nilitoka tumboni kwa sababu gani, kuona taabu na huzuni, hata siku zangu ziharibike katika aibu?
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.