Yobu 5:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwani taabu haitoki mchangani, Wala mashaka hayachipuki katika nchi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa kawaida mateso hayatoki mavumbini wala matatizo hayachipui udongoni. Biblia Habari Njema - BHND Kwa kawaida mateso hayatoki mavumbini wala matatizo hayachipui udongoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa kawaida mateso hayatoki mavumbini wala matatizo hayachipui udongoni. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana taabu haioti kutoka kwa udongo, wala ubaya hauchipui kutoka ardhini. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo, wala udhia hauchipui kutoka ardhini. BIBLIA KISWAHILI Kwani taabu haitoki mchangani, Wala mashaka hayachipuki katika nchi; |
Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;
Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba.
Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi.
Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?
Isipokuwa niliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala BWANA hakuyafanya haya yote.
mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Kisha angalieni, likikwea kwa njia ya mpakani mwake kwenda Beth-shemeshi, basi, ndiye aliyetutenda uovu huo mkuu; la, sivyo, ndipo tutakapojua ya kwamba si mkono wake uliotupiga; ilikuwa ni bahati mbaya iliyotupata.