Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.
Yobu 5:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utakingwa salama na mashambulio ya ulimi, wala hutaogopa maangamizi yajapo. Biblia Habari Njema - BHND Utakingwa salama na mashambulio ya ulimi, wala hutaogopa maangamizi yajapo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utakingwa salama na mashambulio ya ulimi, wala hutaogopa maangamizi yajapo. Neno: Bibilia Takatifu Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia. Neno: Maandiko Matakatifu Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia. BIBLIA KISWAHILI Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja. |
Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.
Utawasitiri kutoka kwa fitina za watu Katika maficho ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na ushindani wa ndimi.
BWANA ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu nilipozongwa kama mji wenye boma.
Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.