Mungu alinituma mbele yenu kuwahifadhia mabaki katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.
Yobu 5:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati wa njaa atakuokoa na kifo, katika mapigano makali atakuokoa. Biblia Habari Njema - BHND Wakati wa njaa atakuokoa na kifo, katika mapigano makali atakuokoa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati wa njaa atakuokoa na kifo, katika mapigano makali atakuokoa. Neno: Bibilia Takatifu Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga. BIBLIA KISWAHILI Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga. |
Mungu alinituma mbele yenu kuwahifadhia mabaki katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.
Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.
Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumainia BWANA.
Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumlipa Mungu fidia kwa ajili ya maisha yake,
BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
Ndipo Sedekia mfalme akatoa amri, wakamtia Yeremia katika ukumbi wa walinzi; wakampa kila siku mkate mmoja uliotoka katika njia ya waokaji, hata mkate wote wa mji ulipokwisha. Basi Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi.
Kwa maana ni yakini, nitakuokoa, wala hutaanguka kwa upanga, lakini nafsi yako itakuwa kama nyara kwako; kwa kuwa ulinitumaini mimi, asema BWANA.
Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.
Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe;
Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.