Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea dada yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.
Yobu 5:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ama kweli hangaiko humuua mpumbavu, na wivu humwangamiza mjinga. Biblia Habari Njema - BHND Ama kweli hangaiko humuua mpumbavu, na wivu humwangamiza mjinga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ama kweli hangaiko humuua mpumbavu, na wivu humwangamiza mjinga. Neno: Bibilia Takatifu Kuweka uchungu moyoni humuua mpumbavu, nao wivu humchinja mjinga. Neno: Maandiko Matakatifu Kuweka uchungu moyoni humuua mpumbavu, nao wivu humchinja mjinga. BIBLIA KISWAHILI Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga. |
Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea dada yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.
Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, alimwaga mbegu chini asimpe nduguye uzao.
Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake?
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.
Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.
Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru.
Mungu akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa.
na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu;
Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za kila namna;