Yobu 5:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwani yeye huumiza na pia huuguza; hujeruhi, na kwa mkono wake huponya. Biblia Habari Njema - BHND Kwani yeye huumiza na pia huuguza; hujeruhi, na kwa mkono wake huponya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwani yeye huumiza na pia huuguza; hujeruhi, na kwa mkono wake huponya. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; huumiza, lakini mikono yake pia huponya. BIBLIA KISWAHILI Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya. |
Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya.
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.
Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.
Kisha kuhani akiingia ndani kukagua na kuona kuwa pigo halikuenea katika hiyo nyumba baada ya nyumba kupakwa chokaa; ndipo kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi, maana pigo limepoa.
Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,