Yobu 5:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Heri mtu yule ambaye Mungu anamrudi! Hivyo usidharau Mungu Mwenye Nguvu anapokuadhibu. Biblia Habari Njema - BHND “Heri mtu yule ambaye Mungu anamrudi! Hivyo usidharau Mungu Mwenye Nguvu anapokuadhibu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Heri mtu yule ambaye Mungu anamrudi! Hivyo usidharau Mungu Mwenye Nguvu anapokuadhibu. Neno: Bibilia Takatifu “Heri mtu yule ambaye Mungu humkanya; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi. Neno: Maandiko Matakatifu “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi. BIBLIA KISWAHILI Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi. |
Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake, Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu.
Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana kizuizi; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.
Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoea nira; unigeuze, nami nitageuka; kwa maana wewe u BWANA, Mungu wangu.
Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo BWANA, Mungu wako, akurudivyo.
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
Angalieni, twawaita heri wao waliostahimili. Mmesikia habari za kustahimili kwake Ayubu, kuona mwisho Bwana aliyomtendea, jinsi Bwana alivyo mwingi wa rehema na mwenye huruma.