Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
Yobu 5:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwanasa wenye hekima kwa werevu wao, mipango ya wajanja huikomesha mara moja. Biblia Habari Njema - BHND Huwanasa wenye hekima kwa werevu wao, mipango ya wajanja huikomesha mara moja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwanasa wenye hekima kwa werevu wao, mipango ya wajanja huikomesha mara moja. Neno: Bibilia Takatifu Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali. BIBLIA KISWAHILI Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. |
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.
bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba huo mpango mwovu alioufanya juu ya Wayahudi umrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti.
Na roho yao Misri itaondolewa, nami nitaiharibu mipango yao, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli na kwa wachawi.
Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na Torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la BWANA, wana akili gani ndani yao?
Nena, BWANA asema hivi, Mizoga ya watu itaanguka kama samadi juu ya mashamba, Na kama konzi ya ngano nyuma yake avunaye, wala hapana mtu atakayeikusanya.
Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajisukuma ukutani, akaubana mguu wake Balaamu, basi akampiga mara ya pili.
Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.