Yobu 5:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwainua juu walio wanyonge, wenye kuomboleza huwapa usalama. Biblia Habari Njema - BHND Huwainua juu walio wanyonge, wenye kuomboleza huwapa usalama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwainua juu walio wanyonge, wenye kuomboleza huwapa usalama. Neno: Bibilia Takatifu Huwainua juu wanyonge, nao wale wanaoomboleza huinuliwa wakawa salama. Neno: Maandiko Matakatifu Huwainua juu wanyonge, nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama. BIBLIA KISWAHILI Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama. |
Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.
Lakini alimwinua mhitaji juu mbali na mateso, Na kuwaongeza jamaa zao kama kundi la kondoo.
Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.
Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.
Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.