Yobu 5:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huinyeshea nchi mvua, hupeleka maji mashambani. Biblia Habari Njema - BHND Huinyeshea nchi mvua, hupeleka maji mashambani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huinyeshea nchi mvua, hupeleka maji mashambani. Neno: Bibilia Takatifu Yeye huipa nchi mvua, huyapeleka maji kunyesha mashamba. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye huipa nchi mvua, huyapeleka maji kunyesha mashamba. BIBLIA KISWAHILI Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani; |
Kwa kuwa huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na pia kwa manyunyu ya mvua, Hayo manyunyu ya mvua yake nyingi.
Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.
Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche BWANA, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea majuma ya mavuno yaliyoamriwa.
Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikauka.
Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha.