Yobu 42:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni nani huyu afichaye ushauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga. Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewa mambo ya ajabu mno kwangu ambayo sikuwa ninayajua. Biblia Habari Njema - BHND Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga. Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewa mambo ya ajabu mno kwangu ambayo sikuwa ninayajua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga. Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewa mambo ya ajabu mno kwangu ambayo sikuwa ninayajua. Neno: Bibilia Takatifu Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ Hakika nilisema mambo nisiyoyaelewa, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua. Neno: Maandiko Matakatifu Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua. BIBLIA KISWAHILI Ni nani huyu afichaye ushauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. |
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.