Yobu 41:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Pumzi zake huwasha makaa, Na miali ya moto hutoka kinywani mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwake, rungu ni kama kipande cha bua, hucheka likitupiwa fumo kwa wingi. Biblia Habari Njema - BHND Kwake, rungu ni kama kipande cha bua, hucheka likitupiwa fumo kwa wingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwake, rungu ni kama kipande cha bua, hucheka likitupiwa fumo kwa wingi. Neno: Bibilia Takatifu Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake. Neno: Maandiko Matakatifu Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake. BIBLIA KISWAHILI Pumzi zake huwasha makaa, Na miali ya moto hutoka kinywani mwake. |
Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Kukapita mawingu yake makuu. Ikashuka mvua ya mawe na makaa ya moto.
Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto wa kuteketeza ukatoka kinywani mwake, Makaa ya moto yakamtoka.
Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuri yake ni moto na kuni nyingi; pumzi ya BWANA, kama mto wa kiberiti, huiwasha.
Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.