Yobu 40:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Je, wewe mwenye kuchunguza makosa utashindana na Mungu Mwenye Nguvu? Wewe unayebishana nami Mungu, basi jibu mambo hayo!” Biblia Habari Njema - BHND “Je, wewe mwenye kuchunguza makosa utashindana na Mungu Mwenye Nguvu? Wewe unayebishana nami Mungu, basi jibu mambo hayo!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Je, wewe mwenye kuchunguza makosa utashindana na Mungu Mwenye Nguvu? Wewe unayebishana nami Mungu, basi jibu mambo hayo!” Neno: Bibilia Takatifu “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.” Neno: Maandiko Matakatifu “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.” BIBLIA KISWAHILI Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye. |
Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!
Na awe kitu chochote, aliitwa jina lake zamani za kale, naye amejulikana kuwa ndiye mwanadamu; wala hawezi kabisa kushindana na yeye aliye na uwezo kuliko yeye mwenyewe.
Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonesha njia ya fahamu?
Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na anikaribie basi.
Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.
Je! Maana yake ni nini hata mkatumia mithali hii katika Israeli, mkisema, Baba wamekula zabibu mbichi, nao watoto wakatiwa ganzi la meno?
Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.