Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia uvumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.
Yobu 4:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu huwaangamiza hao kwa pumzi yake, hao huteketezwa kwa pigo la hasira yake. Biblia Habari Njema - BHND Mungu huwaangamiza hao kwa pumzi yake, hao huteketezwa kwa pigo la hasira yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu huwaangamiza hao kwa pumzi yake, hao huteketezwa kwa pigo la hasira yake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; kwa mshindo wa hasira zake huangamia. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; kwa mshindo wa hasira zake huangamia. BIBLIA KISWAHILI Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika. |
Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia uvumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.
mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Hataondoka gizani; Ndimi za moto zitayakausha matawi yake, Naye ataondoka kwa pumzi za kinywa chake.
Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee BWANA, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.
Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa kilima, Vilindi vikagandamana katikati ya bahari.
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuri yake ni moto na kuni nyingi; pumzi ya BWANA, kama mto wa kiberiti, huiwasha.
Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake;
Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.