Yobu 4:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nijuavyo mimi, wapandao uovu na ubaya huvuna hayohayo, Biblia Habari Njema - BHND Nijuavyo mimi, wapandao uovu na ubaya huvuna hayohayo, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nijuavyo mimi, wapandao uovu na ubaya huvuna hayohayo, Neno: Bibilia Takatifu Kwa jinsi mimi nimechunguza, wale walimao ubaya na wale hupanda uovu, huvuna hayo hayo. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza, wale walimao ubaya na wale hupanda uovu, huvuna hayo hayo. BIBLIA KISWAHILI Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo. |
Katika siku ile ulipopanda, ulifanya kitalu, na wakati wa asubuhi ulizimeesha mbegu zako, lakini mavuno yatatoweka siku ya huzuni, na ya sikitiko la moyo lifishalo.
Njia yako na matendo yako yamekupatia haya; huu ndio uovu wako; kwa maana ni uchungu, hakika unafikia hata moyo wako.
Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.
Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.