Yobu 4:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Fikiri sasa: Nani asiye na hatia ambaye amepata kuangamia? Au, je, waadilifu wamepata kutupwa? Biblia Habari Njema - BHND Fikiri sasa: Nani asiye na hatia ambaye amepata kuangamia? Au, je, waadilifu wamepata kutupwa? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Fikiri sasa: nani asiye na hatia ambaye amepata kuangamia? Au, je, waadilifu wamepata kutupwa? Neno: Bibilia Takatifu “Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa? Neno: Maandiko Matakatifu “Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa? BIBLIA KISWAHILI Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali? |
Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.
Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.
Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewalewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.
basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;