Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
Yobu 4:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Dini yako siyo tegemeo lako? Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako? Na unyofu wako si ndilo tumaini lako? Biblia Habari Njema - BHND Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako? Na unyofu wako si ndilo tumaini lako? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako? Na unyofu wako si ndilo tumaini lako? Neno: Bibilia Takatifu Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa ndiyo matumaini yako na njia zako kutokuwa na lawama ndilo taraja lako? Neno: Maandiko Matakatifu Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa ndiyo matumaini yako na njia zako kutokuwa na lawama ndilo taraja lako? BIBLIA KISWAHILI Je! Dini yako siyo tegemeo lako? Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? |
Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumainia BWANA.
Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.
Kwa hiyo iweni tayari, na makini; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.