Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yobu 4:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Maneno yako yamewainua waliokufa moyo, umewaimarisha waliokosa nguvu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Maneno yako yamewainua waliokufa moyo, umewaimarisha waliokosa nguvu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Maneno yako yamewainua waliokufa moyo, umewaimarisha waliokosa nguvu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa; umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa; umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yobu 4:4
15 Marejeleo ya Msalaba  

Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia.


Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.


Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.


Lakini sasa haya yamekufikia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika.


BWANA huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini.


Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.


Neno linenwalo wakati ufaao, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.


Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.


Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.


hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi.


Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito.


Ndugu, tunawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.


Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,