Yobu 4:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Kamba ya hema yao haikung'olewa ndani yao? Nao hufa hata bila kuwa na hekima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Iwapo uzi unaoshikilia uhai wao ukikatwa wao hufa tena bila kuwa na hekima. Biblia Habari Njema - BHND Iwapo uzi unaoshikilia uhai wao ukikatwa wao hufa tena bila kuwa na hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Iwapo uzi unaoshikilia uhai wao ukikatwa wao hufa tena bila kuwa na hekima. Neno: Bibilia Takatifu Je, kamba za hema lao hazikung’olewa, hivyo hufa bila hekima?’ Neno: Maandiko Matakatifu Je, kamba za hema yao hazikung’olewa, hivyo hufa bila hekima?’ BIBLIA KISWAHILI Je! Kamba ya hema yao haikung'olewa ndani yao? Nao hufa hata bila kuwa na hekima. |
Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili.
Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu.
Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;
Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake iko katika mianzi ya pua yake; kwa maana wanafaa kitu gani?
Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.