Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yobu 4:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao wanaopondwa kama nondo!

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

sembuse binadamu viumbe vya udongo, watu ambao chanzo chao ni mavumbi, ambao waweza kupondwapondwa kama nondo!

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

sembuse binadamu viumbe vya udongo, watu ambao chanzo chao ni mavumbi, ambao waweza kupondwapondwa kama nondo!

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

sembuse binadamu viumbe vya udongo, watu ambao chanzo chao ni mavumbi, ambao waweza kupondwapondwa kama nondo!

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

ni mara ngapi zaidi wale wanaoishi katika nyumba za udongo wa mfinyanzi, ambazo misingi yake ipo mavumbini, ambao wamepondwa kama nondo!

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba za udongo wa mfinyanzi, ambazo misingi yake ipo mavumbini, ambao wamepondwa kama nondo!

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao wanaopondwa kama nondo!

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yobu 4:19
18 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.


BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.


kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.


Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?


Maneno yenu ya hekima ni mithali ya majivu, Ngome zenu ni ngome za udongo.


Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.


Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.


Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao, Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji;


Seuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!


Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.


Pumzi yake inapomtoka, anarudi katika udongo wake, Siku iyo hiyo mipango yake hutoweka.


Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili.


Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.


Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.


Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.


Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;