Yobu 4:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Upepo ukapita mbele ya uso wangu, nywele za mwilini mwangu zikajisimamisha. Biblia Habari Njema - BHND Upepo ukapita mbele ya uso wangu, nywele za mwilini mwangu zikajisimamisha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Upepo ukapita mbele ya uso wangu, nywele za mwilini mwangu zikajisimamisha. Neno: Bibilia Takatifu Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu, nazo nywele za mwili wangu zikasimama. Neno: Maandiko Matakatifu Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu, nazo nywele za mwili wangu zikasimama. BIBLIA KISWAHILI Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. |
Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,
Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame wima; maana nimetumwa kwako sasa. Na aliponiambia neno hili, nilisimama nikitetemeka.
Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.
Wanafunzi walipomwona akitembea juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni mzimu; wakapiga yowe kwa hofu.
Na kuhusu malaika asema, Awafanya malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.