Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
Yobu 4:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hofu iliniangukia na kutetemeka, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema nilishikwa na hofu na kutetemeka, mifupa yangu yote ikagonganagongana. Biblia Habari Njema - BHND nilishikwa na hofu na kutetemeka, mifupa yangu yote ikagonganagongana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza nilishikwa na hofu na kutetemeka, mifupa yangu yote ikagonganagongana. Neno: Bibilia Takatifu hofu na kutetemeka kulinishika na kufanya mifupa yangu yote itetemeke. Neno: Maandiko Matakatifu hofu na kutetemeka kulinishika na kufanya mifupa yangu yote itetemeke. BIBLIA KISWAHILI Hofu iliniangukia na kutetemeka, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. |
Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.
Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.
Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame wima; maana nimetumwa kwako sasa. Na aliponiambia neno hili, nilisimama nikitetemeka.
Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.
Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,