Yobu 4:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Siku moja, niliambiwa neno kwa siri, sikio langu lilisikia mnongono wake. Biblia Habari Njema - BHND “Siku moja, niliambiwa neno kwa siri, sikio langu lilisikia mnongono wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Siku moja, niliambiwa neno kwa siri, sikio langu lilisikia mnong'ono wake. Neno: Bibilia Takatifu “Neno lililetwa kwangu kwa siri, masikio yangu yakasikia mnong’ono wake. Neno: Maandiko Matakatifu “Neno lililetwa kwangu kwa siri, masikio yangu yakasikia mnong’ono wake. BIBLIA KISWAHILI Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake. |
Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?
Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiapo watu, Katika usingizi kitandani;
Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.