Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?
Yobu 4:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba jike wametawanyika mbalimbali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Simba mwenye nguvu hufa kwa kukosa mawindo, na watoto wa simba jike hutawanywa! Biblia Habari Njema - BHND Simba mwenye nguvu hufa kwa kukosa mawindo, na watoto wa simba jike hutawanywa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Simba mwenye nguvu hufa kwa kukosa mawindo, na watoto wa simba jike hutawanywa! Neno: Bibilia Takatifu Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo, nao wana wa simba jike hutawanyika. Neno: Maandiko Matakatifu Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo, nao wana wa simba jike hutawanyika. BIBLIA KISWAHILI Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba jike wametawanyika mbalimbali. |
Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?
mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.
Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa; ameanza kushika njia, ametoka katika mahali pake; ili aifanye nchi yako kuwa ukiwa, miji yako ifanywe maganjo, asibaki mwenyeji ndani yake.
Watakwenda kumfuata BWANA, atakayenguruma kama simba; kwa maana atanguruma, nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka.
Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.
Aliinama, akalala mfano wa simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha? Na abarikiwe kila akubarikiye, Na alaaniwe kila akulaaniye.
Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba.