Yobu 39:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hujitenga kabisa na makelele ya miji, hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi. Biblia Habari Njema - BHND Hujitenga kabisa na makelele ya miji, hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hujitenga kabisa na makelele ya miji, hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi. Neno: Bibilia Takatifu Huzicheka ghasia za mji, wala hasikii kelele za mwendesha gari. Neno: Maandiko Matakatifu Huzicheka ghasia za mji, wala hasikii kelele za mwendesha gari. BIBLIA KISWAHILI Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi. |
Basi, nendeni sasa, mkafanye kazi; kwa maana hamtapewa majani, na pamoja na hayo mtaleta hesabu ile ile ya matofali.
Maana BWANA aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwanasimba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo BWANA wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.
Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.