Yobu 39:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kiota chake mahali pa juu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, tai hupaa juu kwa amri yako, na kuweka kiota chake juu milimani? Biblia Habari Njema - BHND Je, tai hupaa juu kwa amri yako, na kuweka kiota chake juu milimani? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, tai hupaa juu kwa amri yako, na kuweka kiota chake juu milimani? Neno: Bibilia Takatifu Je, tai hupaa juu kwa amri yako na kujenga kiota chake mahali pa juu? Neno: Maandiko Matakatifu Je, tai hupaa juu kwa amri yako na kujenga kiota chake mahali pa juu? BIBLIA KISWAHILI Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kiota chake mahali pa juu? |
Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi.
Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.
bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelivunja agano langu, wameiasi sheria yangu.
Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu;
Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kiota chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.