Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.
Yobu 38:41 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni nani awapaye kunguru chakula chao, makinda yao yanaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na huko kwa njaa? Biblia Habari Njema - BHND Ni nani awapaye kunguru chakula chao, makinda yao yanaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na huko kwa njaa? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni nani awapaye kunguru chakula chao, makinda yao yanaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na huko kwa njaa? Neno: Bibilia Takatifu Ni nani ampaye kunguru chakula wakati makinda yake yanamlilia Mungu, yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula? Neno: Maandiko Matakatifu Ni nani ampaye kunguru chakula wakati makinda yake yanamlilia Mungu, yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula? BIBLIA KISWAHILI Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula? |
Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!