Yobu 38:34 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawingu yakufunike kwa mtiririko wa mvua? Biblia Habari Njema - BHND “Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawingu yakufunike kwa mtiririko wa mvua? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawingu yakufunike kwa mtiririko wa mvua? Neno: Bibilia Takatifu “Unaweza kuipaza sauti yako hadi mawinguni, na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji? Neno: Maandiko Matakatifu “Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji? BIBLIA KISWAHILI Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize? |
Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni?
mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake;
Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA aletaye mawingu ya mvua, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi shambani.
Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akatuma ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia.