Yobu 38:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ipi njia ya kwenda mahali mwanga unapogawanywa, au huko kunakotoka upepo wa mashariki ukasambazwa duniani? Biblia Habari Njema - BHND Ipi njia ya kwenda mahali mwanga unapogawanywa, au huko kunakotoka upepo wa mashariki ukasambazwa duniani? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ipi njia ya kwenda mahali mwanga unapogawanywa, au huko kunakotoka upepo wa mashariki ukasambazwa duniani? Neno: Bibilia Takatifu Njia iendayo mahali miali ya radi inapotawanywa ni ipi, au njia iendayo mahali upepo wa mashariki unaposambazwa juu ya dunia? Neno: Maandiko Matakatifu Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa, au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia? BIBLIA KISWAHILI Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi? |
Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika.
Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akatayarisha upepo wa mashariki, wenye joto jingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.