Yobu 38:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Je, makao ya mwanga yako wapi? Nyumbani kwa giza ni wapi, Biblia Habari Njema - BHND “Je, makao ya mwanga yako wapi? Nyumbani kwa giza ni wapi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Je, makao ya mwanga yako wapi? Nyumbani kwa giza ni wapi, Neno: Bibilia Takatifu “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako maskani mwa giza ni wapi? Neno: Maandiko Matakatifu “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako maskani mwa giza ni wapi? BIBLIA KISWAHILI Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? |
Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Akiwa katika giza la mawingu mazito yaliyojaa maji.
Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
Mianga yote ya mbinguni iangazayo nitaifanya kuwa giza juu yako, nami nitatia giza katika nchi yako, asema Bwana MUNGU.
Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.