Lakini watu hawa ni wengi, tena ni wakati wa mvua nyingi, nasi hatuwezi kusimama nje, tena kazi hii si kazi ya siku moja, wala ya siku mbili; maana tumekosa sana katika jambo hili.
Yobu 37:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na pia kwa manyunyu ya mvua, Hayo manyunyu ya mvua yake nyingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya nchi!’ Na manyunyu na mvua, ‘Nyesha kwa nguvu.’ Biblia Habari Njema - BHND Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya nchi!’ Na manyunyu na mvua, ‘Nyesha kwa nguvu.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya nchi!’ na manyunyu na mvua, ‘Nyesha kwa nguvu.’ Neno: Bibilia Takatifu Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’ Neno: Maandiko Matakatifu Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’ BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na pia kwa manyunyu ya mvua, Hayo manyunyu ya mvua yake nyingi. |
Lakini watu hawa ni wengi, tena ni wakati wa mvua nyingi, nasi hatuwezi kusimama nje, tena kazi hii si kazi ya siku moja, wala ya siku mbili; maana tumekosa sana katika jambo hili.
Ndipo wanaume wote wa Yuda na Benyamini wakakusanyika katika muda wa siku tatu; ulikuwa mwezi wa tisa, siku ya ishirini ya mwezi; na watu wote wakaketi katika uwanja, mbele ya nyumba ya Mungu, wakitetemeka kwa sababu ya neno hilo, na kwa sababu ya mvua kubwa.
basi waambie hao wanaoupaka ukuta chokaa isiyokorogwa vema, ya kwamba utaanguka; kutakuwa mvua ya kufurika; nanyi, enyi mvua ya mawe makubwa ya barafu, mtaanguka; na upepo wa dhoruba utaupasua.
Basi Bwana MUNGU asema hivi; Nitaupasua kwa upepo wa dhoruba, katika ghadhabu yangu; tena kutakuwa mvua ya barafu ya kufurika katika hasira yangu; na mawe makubwa ya barafu katika hasira ya kuukomesha.
Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake.