Yobu 37:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikilizeni ngurumo ya sauti ya Mungu, na mvumo wa sauti kutoka kinywani mwake. Biblia Habari Njema - BHND Sikilizeni ngurumo ya sauti ya Mungu, na mvumo wa sauti kutoka kinywani mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikilizeni ngurumo ya sauti ya Mungu, na mvumo wa sauti kutoka kinywani mwake. Neno: Bibilia Takatifu Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, sauti ya ngurumo inayotoka kinywani mwake. Neno: Maandiko Matakatifu Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake. BIBLIA KISWAHILI Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake. |
Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa.
Atoapo sauti yake pana kishindo cha maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.