Yobu 37:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Unapaswa kusikiliza Yobu; nyamaza, usikilize maajabu ya Mungu. Biblia Habari Njema - BHND “Unapaswa kusikiliza Yobu; nyamaza, usikilize maajabu ya Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Unapaswa kusikiliza Yobu; nyamaza, usikilize maajabu ya Mungu. Neno: Bibilia Takatifu “Ayubu, sikiliza hili; nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu “Ayubu, sikiliza hili; nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu. BIBLIA KISWAHILI Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. |
Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa.
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.