Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yobu 37:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake, Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mungu hutekeleza matakwa yake duniani; iwe ni kwa ajili ya kuwaadhibu watu, au kwa ajili ya kuonesha upendo wake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mungu hutekeleza matakwa yake duniani; iwe ni kwa ajili ya kuwaadhibu watu, au kwa ajili ya kuonesha upendo wake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mungu hutekeleza matakwa yake duniani; iwe ni kwa ajili ya kuwaadhibu watu, au kwa ajili ya kuonesha upendo wake.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu, au kuinyeshea dunia yake na kuonesha upendo wake.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu, au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake, Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yobu 37:13
14 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hadi waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku.


Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi.


Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele.


Ikawa, muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanyesha mvua nyingi. Ahabu akapanda garini, akaenda zake Yezreeli.


Ndipo wanaume wote wa Yuda na Benyamini wakakusanyika katika muda wa siku tatu; ulikuwa mwezi wa tisa, siku ya ishirini ya mwezi; na watu wote wakaketi katika uwanja, mbele ya nyumba ya Mungu, wakitetemeka kwa sababu ya neno hilo, na kwa sababu ya mvua kubwa.


Kwani huwahukumu makabila ya watu kwa njia hizi; Hutoa chakula kwa ukarimu.


Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.


Kwa kuwa huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na pia kwa manyunyu ya mvua, Hayo manyunyu ya mvua yake nyingi.


Matuta yake wayajaza maji; Wapasawazisha palipoinuka, Wailainisha nchi kwa manyunyu; Waibariki mimea yake.


Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama awali.