Yobu 37:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wangu hutetemeka kwa hayo pia, Nao huruka kutoka mahali pake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kutokana na hayo, moyo wangu unatetemeka, na kuruka kutoka mahali pake. Biblia Habari Njema - BHND “Kutokana na hayo, moyo wangu unatetemeka, na kuruka kutoka mahali pake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kutokana na hayo, moyo wangu unatetemeka, na kuruka kutoka mahali pake. Neno: Bibilia Takatifu “Kwa hili moyo wangu unatetemeka, nao unaruka kutoka mahali pake. Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa hili moyo wangu unatetemeka, nao unaruka kutoka mahali pake. BIBLIA KISWAHILI Moyo wangu hutetemeka kwa hayo pia, Nao huruka kutoka mahali pake. |
Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.
Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.
Ghafla pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.