Yobu 35:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa sababu ya wingi wa dhuluma wao hulia; Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kwa sababu ya udhalimu mwingi watu hulia, huomba msaada kwa sababu ya mapigo ya wenye nguvu. Biblia Habari Njema - BHND “Kwa sababu ya udhalimu mwingi watu hulia, huomba msaada kwa sababu ya mapigo ya wenye nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kwa sababu ya udhalimu mwingi watu hulia, huomba msaada kwa sababu ya mapigo ya wenye nguvu. Neno: Bibilia Takatifu “Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso; huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu “Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso; huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu. BIBLIA KISWAHILI Kwa sababu ya wingi wa dhuluma wao hulia; Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu. |
Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang'anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.
Watu huugua toka mji ulio na watu wengi, Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele; Wala Mungu hauangalii upumbavu.
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
Na kisha baada ya muda, yule mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
Ukiwatesa watu hao katika neno lolote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.
mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.