Yobu 35:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hakika Mungu hatasikia ubatili, Wala Mwenyezi hatauangalia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli Mungu hasikilizi kilio cha bure; Mungu Mwenye Nguvu hajali kilio hicho. Biblia Habari Njema - BHND Kweli Mungu hasikilizi kilio cha bure; Mungu Mwenye Nguvu hajali kilio hicho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli Mungu hasikilizi kilio cha bure; Mungu Mwenye Nguvu hajali kilio hicho. Neno: Bibilia Takatifu Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; Mwenyezi hayazingatii. Neno: Maandiko Matakatifu Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; Mwenyezi hayazingatii. BIBLIA KISWAHILI Hakika Mungu hatasikia ubatili, Wala Mwenyezi hatauangalia. |
Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, lakini sitawasikiliza.
Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.
Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.
Ndipo watakapomwomba BWANA, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao.
Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.