Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo BWANA alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,
Yobu 34:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu? Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona, Biblia Habari Njema - BHND Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu? Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu? Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona, Neno: Bibilia Takatifu Lakini akikaa kimya, ni nani awezaye kumhukumu? Akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumwona? Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kama akinyamaza kimya, ni nani awezaye kumhukumu? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumwona? Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa, BIBLIA KISWAHILI Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa; |
Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo BWANA alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,
naam, kama ilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena BWANA anakuambia ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.
Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena; Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.
Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza? Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.
Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Usinifiche uso wako, Usimkatalie mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
BWANA, kwa radhi yako Wewe uliuimarisha mlima wangu. Uliuficha uso wako, Nami nikafadhaika.
Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
Na itakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka kumtumikia Nebukadneza, huyo mfalme wa Babeli, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, asema BWANA, hata nitakapokuwa nimewaangamiza kwa mkono wake.
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.