Akampa jina BWANA aliyesema naye, “Wewe U Mungu uonaye,” kwani alisema, “Kweli nimemwona Mungu na nikaendelea kuishi baada ya kumuona?”
Yobu 34:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwani macho yake yako juu ya njia za mtu, Naye huziona hatua zake zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu; yeye huziona hatua zao zote. Biblia Habari Njema - BHND “Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu; yeye huziona hatua zao zote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu; yeye huziona hatua zao zote. Neno: Bibilia Takatifu “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao. Neno: Maandiko Matakatifu “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao. BIBLIA KISWAHILI Kwani macho yake yako juu ya njia za mtu, Naye huziona hatua zake zote. |
Akampa jina BWANA aliyesema naye, “Wewe U Mungu uonaye,” kwani alisema, “Kweli nimemwona Mungu na nikaendelea kuishi baada ya kumuona?”
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote, hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.
mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,
Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema BWANA.