BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Yobu 33:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Roho ya Mungu iliniumba, nayo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu yanipa uhai. Biblia Habari Njema - BHND Roho ya Mungu iliniumba, nayo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu yanipa uhai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Roho ya Mungu iliniumba, nayo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu yanipa uhai. Neno: Bibilia Takatifu Roho wa Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. Neno: Maandiko Matakatifu Roho wa Mwenyezi Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. BIBLIA KISWAHILI Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. |
BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.
Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa kiumbe aliye hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.